“Diana anawapotosha wasichana wadogo” – Nyota Ndogo

Msaani Nyota Ndogo amewataka Dj Mo na size 8 na Diana kupunguza kufanya kiki zisizokuwa na msingi kwa minajili ya kupata ufuasi katika mitandao ya kijamii.

 Akizungumza kwenye kipindi cha mashav mashav  akiwa na Ken1gb, Nyota Ndogo amesmea kuwa vitu mabavyo wawili hao wamekuwa wakifanya hivi karibuni vimepita mipaka.

 “Alichokizungumza jana Diana na kitu ambacho hakifai kusemwa yeye kusema kuwa amewahi kutoka na wanaume wengi na pia kumdate mume wa mtu sio sawa” alisema Nyota Ndogo

“Anawapa picha mabaya wasichana wadogo amabao kwa sasa wanadhani kuwa kuwadate wanaume wengi ndio njia rahisi ya kupata hela”  alisema Nyota ndogo.

Vile vile Nyota Ndogo aliwakosoa Dj Mo na Size 8 akisema njia wanayotumia kutafuta ufuasi mtandaoni huenda ikawaletea msomgo wa mawazo kutokana na maneno ambayo watu wanaongea kwenye mtandao.

Kuhusu kibao chake kipya Nyota ndogo amesema kuwa aliamua kumhusisha Kelechi Africana katika Uwandishi wa kazi yake kwa sababu alikuwa nalenga vijana na wasasa.

Pia amewataka wasaani wachanga wenye uwezo wa kuandika kujitokeza na kufanya naye kazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *