Deni la Barcelona la fika Bilioni 1 hawajui la kufanya

Deni la Zaidi ya euro bilioni 1 inayodaiwa club ya Barcelona  huenda ikaiwacha club hio katika hatari kubwa siku za Usoni.

Miamba hao wa soka wa eneo la Catalunya wanapitia wakati mgumu kulipa madeni yao ambao yamegonga dola billioni moja huku ikibainika kuwa janga la Corona ndilo lilichnagia kupanda maradfu kwa deni la Barcelona.

Kwa mujibu wa Jarida la Catalunya la Vangundia ni kuwa Barcelona wanafaa kulipa deni la euro millioni 420 kwa kipindi cha muda wa miezi 12 ijao.

Kwa sasa tayari Barcelona ishatumia asilimia 70 ya bajeti yake ya kila mwaka kulipia mishahara na kuwanunua wachezaji. Kote duniaani Barcelona ndio club inayotumiwa fedha nyingi kuwalipa mshahara wachezaji wakiwa wanatuma euro millioni 485 kila mwaka.

Kwa mjibu wa reporti barcelona hupata euro millioni 320 kutokana na mashabiki wake kuzuri uwanja wa Nou camp ambako pia panapatikana makavazi ya Barcelona.

Kwa sasa baadhi ya marupurupu wanayo pokea wachezaji wa Barcelona imesitishwa kwa muda hadi pale mashabiki watakapo ruhusiwa kurejea tena viwanjani.

Kando na Barcelona Mashetani Wekundu Manchester United ndio club ya soka inayotajwa kuwa na deni kubwa duniani wakiwa wanadaiwa ueuro millioni 568 licha ya kushikilia nafasi ya 3 miongoni mwa vilabu tajiri duniani.

 Deni la Manchester United liliongezeka mara dufu toka mwaka 2005 baada ya kununuliwa na Familia ya Glazer toka nchini Marekani ambao inadaiwa kuwa walitumia club ya Manchester united kulipia madeni waliokuwa wanadaiwa katika baishara wanazo zifanya.

Tottenham wanashikilia nafasi ya tatu wakiwa na deni la euro millioni 483 ambalo inatokana na ujenzi wauwanja wao wa Tottenham Stadium ambayo umetajwa kuwa uwanja bora kwa kisasa nchini Ungereza.

Kabla ya kuanza ujenzi wa uwanja huo walichukua mkopo wa Euro millioni 637 katika benki moja nchini marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *