Chama Cha Wiper Chaweka Malengo Ya 2022
Chama cha kisiasa cha Wiper kinalenga kutwa viti zaidi katika bunge la kaunti ya Taita Taveta ikifikia mwaka wa 2022.
katibu wa chama hicho kaunti ya Taita Taveta Peter Shambi anasema kwa sasa wanaendelea kujitayarisha kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao kwa kusajili wanachama zaidi mashinani.
Kaunti ya Taita Taveta imekuwa ngome ya Chama Cha Odm kwa miaka mingi Sasa, nafasi inayoendelea kurithiwa na chama Cha wiper siku za hivi karibuni.
Shambi ameyasema haya baada ya kuapishwa kwa Stephen Mcharo kama mwakilishi wadi ya Wundanyi-Mbale baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi mdogo ulioandaliwa disemba 15 mwaka jana.