Cardinal Becciu,Alazimishwa kujiuzulu kwa tuhuma za ubadhilifu.

Kadinali wa ngazi ya juu Vatican, Giovanni Angelo Becciu amejiuzuru ghafla bila kutarajiwa lakini imebainika kuwa aliambiwa na Papa Francis kufanya hivyo.

Kadinali huyo alishukiwa kutoa fedha ya kanisa na kuwapa ndugu zake ingawa amekanusha kufanya kosa hilo.

Cardinal Becciu alikuwa mshauri wa karibu wa papa na awali katibu wa Vatican.

Alihusika na mkataba ambao una utata wa kuwekeza katika kujenga jengo la kifahari mjini London kwa kutumia fedha za kanisa.

Uwekezaji huo ulikuepo tangu waanze kumfanyia uchunguzi wa matumizi ya fedha.

Mtu kujiuzuru katika ngazi ya ukadinali ni jambo la nadra sana kutokea, taarifa kutoka ofisi ya baba mtakatifu zinasema.

“Baba mtakatifu amekubali maombi ya kujiuzulu yaliyowasilishwa na mwadhama kadinali Giovanni Angelo Becciu.”

Lakini kadinali huyo mwenye umri wa miaka 72, aliuambia mtandao wa Domani nchini Italia kuwa alilazimishwa kujiuzulu kwa sababu alishukiwa kutoa fedha za kanisa kwa kaka zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *