Buriani ‘Papa Shirandula’

Mcheshi na mhusika mashuhuri Charles Bukeko, al maarufu Papa Shirandula alizikwa Jumatatuleo asubuhi nyumbani kwake Nanderema kaunti ndogo ya Funyula,kaunti ya Busia.

Bukeko, afahamikaye zaidi kwa jina lake la kisanii, Papa Shirandula, amejumuishwa kwenye orodha ya waathiriwa walioaga dunia kutokana na ugonjwa wa COVID-19 humu nchini.

Watu 234 wameaga dunia kutokana na COVID-19 nchini huku visa 13,353 vya maambukizi vikiwa zimethibitishwa nchini kufikia Jumapili.

Papa Shirandula aliaga dunia siku ya Ijumaa baada ya kuthibitishwa kuwa na virusi vya corona.

Mkewe Beatrice Andega alisema kuwa Papa aliaga dunia akiwa ndani ya gari kwenye maegesho ya hospitali ya Karen kabla hata ya kulazwa. Bukeko amemwacha mjane na watoto watatu.

Mazishi yake yalitekelezwa na maafisa wa afya ya umma waliokuwa na mavazi maalum kuambatana na kanuni za wizara ya afya kuhusu ugonjwa wa COVID-19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *