Bunge linafaa kupitisha sheria ya usawa wa jinsia,asema Fatuma Achani

Naibu gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani amelitaka bunge la kitaifa kutekeleza wajibu wake wa katiba wa kupitisha mswada wa uwakilishi wa thuluthi mbili wa jinsia.

Akizungumza na wanahabari katika eneo la Ukunda, Achani amesema kuwa bado bunge hilo liko na nafasi ya kupitisha mswada huo.

Kiongozi huyo ametoa changamoto hilo kwa bunge kufuatia ushauri wa jaji mkuu David Maraga kwa rais Uhuru Kenyatta wa kutaka bunge hilo livunjwe.

Aidha, amedokeza kwamba Kenya iko tayari kutekeleza mswada huo wa usawa wa jinsia endapo utapitishwa na bunge.

Ametoa mfano wa utekelezaji wa katiba mpya na mfumo wa ugatuzi uliopitishwa na kukubalika na wakenya wote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *