Bunge La Kaunti Ya Mombasa Latarajiwa Kupitisha Mswada Wa BBI

Bunge la kaunti ya Mombasa linatarajiwa kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba wa BBI hii leo.

Akiongea nje ya bunge la kaunti ya Mombasa mwakilishi wadi mteule Faruma Kushe amesema kuwa hawaupitishi mswada huo kwa kisingizio cha kupokea ruzuku ya shilingi milioni mbili ya magari bali wanaipitisha kwa kuwa inamanufaa mengi mwa wakaazi wa kaunti ya Mombasa.

Naye mwakilishi wadi wa eneo la Shanzu Maimuna Salim amesema waliweza kuchukua maoni ya wananchi na wengi wao waliweza kukubaliana na rasimu hio kikamilifu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *