Boris Johnson anza mkakati ya kubatilisha Brexit

Sheria inayoipa serikali ya waziri mkuu Boris Johnson mamlaka ya kubatilisha makubaliano kuhusu kujiondoa kwa Uingereza kutoka Jumuiya ya Ulaya, imepita kikwazo chake cha kwanza katika bunge la nchi hiyo.

Wabunge 340 waliunga mkono mswada wa masoko ya ndani huku 263 wakiupinga.

Mawaziri wanasema mswada huo una vigezo muhimu vya kulinda jimbo la Northern Ireland na maeneo mengine ya Uingereza ikiwa mashauriano ya mkataba wa kibiashara siku za usoni hautafaulu.

Lakini wapinzani wake wakiwemo baadhi ya wabunge wanaonya kwamba utakuwa na madhara kwa Uingereza kwani unakiuka sheria ya kimataifa.

Viongozi kadhaa mashuhuri wakiwemo aliyekuwa chansela Sajid Javid aliyesusia kura hiyo jana, alisema hawangeunga mkono mswada huo hadi ufanyiwe marekebisho.

Mswada huo unanuiwa kuwezesha utoaji huru wa bidhaa na huduma katika maeneo ya England, Scotland, Wales na Northern Ireland Uingereza itakapoondoka katika soko la Jumuiya ya Ulaya tarehe mosi mwezi Januari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *