Boga na Zani kutoana jasho kwenye kura za mchujo msambweni.

Wagombea wa chama cha ODM kwenye uchaguzi mdogo wa msambweni wamejiandaa kwenye mchujo wa chama hicho utakao fanyika tarehe moja mwezi oktoba  alhamis wiki hii.

Wagombea Omar Boga na Nicholas Zani wanatarajiwa kutoana jasho wakati wa kura za mchujo ambapo atakayeibuka mshindi ndiye atakaye peperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mdogo utakao fanyika mwezi disemba mwaka huu.Hata hivyo wagombea hao wameitaka tume ya uchaguzi na mipaka iebc kutoa orodha ya wapiga kura ya mwaka 2017.

Wameitaka Bodi ya uchaguzi ya odm kuendesha zoezi hilo kwa njia ya uwazi bila ya kuegemea upande wowote wa mgombea.

Aidha wagombea hao wameelezea kile ambacho watakifanya kwa wananchi iwapo watachaguliwa na kuongoza eneo bunge la msambweni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *