Bodaboda Malindi zatakiwa kusitisha kazi wakati wa kafyu

Mwenyekiti wa masuala ya amani na usalama mjini Malindi kaunti ya Kilifi ustadh Athman Said, amewahimiza wahudumu wa boda boda eneo hilo kuhakikisha wanazingatia masaa ya marufuku ya kutoka nje usiku.

Kulingana na Said, kwa sasa idadi kubwa ya wahudumu hao wameonekana kupuuza masharti hayo yanayolenga kupambana na janga la corona.

Mwenyekiti huyo amedai kuwa huenda wahalifu wameanza kutumia fursa hiyo na kupelekea visa vya utovu wa usalama miongono mwa wahudumu hao.

Hata hivyo, amewataka washikadau wa masuala ya uslama kushirikiana ili kukomesha visa vya mauaji kwa wahudumu hao ambavyo vimeanza kuchipuka tena.

Ameonya kuwa yeyote atakayepatikana amejihusisha na uovu huo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *