Bevan: Yasikitisha Watford ilimpiga kalamu Nigel Pearson

Afisa Mkuu wa Chama cha Makocha wa Soka nchini Uingereza Richard Bevan amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba timu ya Watford ilimpiga kalamu kocha wao Nigel Pearson na akatoa mwito kwa vilabu vya soka kuwa na uvumilivu.

Pearson ni Kocha wa tatu kuachishwa kazi katika kilabu hicho cha Watford baada ya kupigwa kalamu kwa Javi Gracia na Quique Sanchez Flores mapema msimuni. Watford inashikilia nafasi ya 18 ikisalia na mechi moja ya kucheza msimu huu na mlindalango Ben Foster amesema kuwa timu hiyo imekosa imani baada ya kufungwa mabao 4-0 Jumanne iliyopita na Manchester City siku mbili baada ya Pearson kupigwa kalamu.

Watford itachuana na Arsenal jumapili hii ikiongozwa na kocha wa muda Hayden Mullins.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *