Bei ya petroli yaongezeka

Bei za petroli zinatarajiwa kuongezeka kwa shilingi 3 na senti 47 kwa lita kuanzia saa sita leo usiku ilhali bei ya mafuta ya Dieseli inatarajiwa kuongezeka kwa shilingi 2 na senti 76 kwa lita.

Watumiaji mafuta taa ndio wapasa kutarajia nyongeza ya juu zaidi ya bei kwa shilingi 18 na senti 20 kwa lita.

Halmashauri ya kudhibiti sekta za kawi na Petroli imetaja nyongeza hizo za bei kusababishwa na kuongezeka kwa bei ya kuagiza mafuta katika muda wa mwezi mmoja uliopita.

Kulingana na taarifa kutoka kwa halmashauri hiyo,lita moja ya mafuta ya Super sasa inatarajiwa kugharimu shilingi 103 na senti 95 jijini Nairobi kutoka kwa bei ya sasa ya shilingi 100 na senti 48.

Mafuta ya Dieseli yanatarajiwa kugharimu shilingi 94 na senti 63 kwa lita kutoka shilingi 91 na senti 87 ilhali bei ya mafuta taa itaongezeka hadi shilingi 83 na senti 65 kwa likta kutoka shilingi 65 na senti 45.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *