Baya asema viongozi kadhaa wamesahau masilahi ya wananchi

Mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya amesema kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa na tamaa ya uongozi na kusahau maslahi ya wananchi waliowachagua.

Akizungumza na meza yetu ya habari Mbunge huyo amesema kuwa baadhi ya viongozi hawajakuwa wakipigania haki za mwananchi na badala yake kuweka tamaa zao mbele jambo ambalo limeathiri kushuhudiwa kwa maendeleo katika eneo hili.


Baya amehoji kuwa wapo baadhi ya viongozi ambao hawajakuwa wakichangia miswada muhimu katika bunge la kitaifa ambayo ametaja kuwa inapania kuimarisha maisha ya mwananchi wa pwani.


Hata hivyo amesema atasimama kidete katika kupigiania kuundwa kwa chama kimoja cha kisiasa cha wapwani iwapo baadhi ya viongozi hawatakubali kuunga mkono swala hilo na kusema kuundwa kwa chama kimoja kitawasaidia wapwani kwani kwa muda wamekuwa wakitelekezwa na vyama vingine kama kile cha ODM punde tu baada ya uchaguzi mkuu kuandaliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *