Baraza la magavana lapigia debe malipo ya kustaafu kwa magavana

Baraza la magavana na kongamano la mabunge ya kaunti zinashinikiza kwa pamoja kuzinduliwa mpango maalum wa malipo ya kustaafu kwa magavana, maspika na wanachama wa mabunge ya kaunti ambao wamehudumu kwa angalau mihula viwili.
Baraza la magavana linaratibu mswada huo wa malipo ya kustaafu ambapo limehimiza mabunge ya kaunti yaunge mkono pendekezo hilo litakalowezesha kubuniwa kwa hazina ya malipo ya ustaafu kwa kaunti.
Mwenyekiti wa baraza la magavana Wycliffe Oparanya na gavana wa Busia Sospeter Ojaamong wamesema pendekezo hilo la baraza la magavana kuhusu maslahi ya magavana, litafanyiwa marekebisho ili kujumuisha maspika na wanachama wa mabunge ya kaunti. 
Ojaamong  alisema maslahi ya wawakilishi wa wadi yanapaswa kupewa kipa umbele ikizingatiwa kwamba wanashirikiana kwa karibu na wapigaji kura.  
Kwa upande wake, Oparanya aliye pia gavana wa Kakamega alisema mradi wa maridhiano almaarufu BBI umeangazia masuala mawili muhimu kwa magatuzi ikiwa ni pamoja na kuelekeza fedha zaidi mashinani na kuzinduliwa kwa hazina ya ustawi wa wadi.   

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *