Bandari Ya Lamu Kuanza Shughuli Zake Mwaka Ujao

Baada ya ujenzi wa badari ya Lamu kusimamishwa kwa muda kutokana na msambao wa virusi vya korona sasa ni rasmi bandari hio itakuwa tayari kuanza shughuli za kupokea meli na shehena za mizigo mwaka ujao.

Akizungumza alipozuru mradi huo mkurugenzi mkuu wa mradi wa LAPSET  Sylvester Kasuku amesema  kuwa kwa sasa mradi huo umekamilika kwa asilimia 80.

Tayari barabara zinazounganisha bandari hio zinaendelea kujengwa na zinatazamiwa kukamilika hivi karibuni.

Kauli hio inajiri baada ya ujumbe wa wakuu wa bandari nchini ukiongozwa na kaimu mkurugenzi wa bandari ya Mombasa Rashid Salimu kuzuru na kukagua hatua zilizopigwa katika ujenzi wa bandari hio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *