Asilimia 78 ya Raia wa Chile Wapiga Kura ya Kuunga Mkono Marekebisho ya Katiba

Raia wa Chile wamepiga kura kuunga mkono kurekebishwa kwa katiba ya nchi hiyo iliyokuwa imepitishwa wakati wa enzi ya utawala wa kiimla wa jenerali Augusto Pinochet. Huku takriban asilimia 90 ya kura zikiwa zimehesabiwa, asilimia  78 ya watu wamepiga kura ya ndiyo kwenye kura ya maamuzi iliyoitishwa kufuatia maandamano ya halaiki dhidi ya ukosefu wa usawa. Rais Sebastian Piñera alipongeza matokeo hayo na kusifu kura hiyo iliyofanyika kwa njia ya amani. Maandamano ya halaiki dhidi ya serikali yalianza nchini Chile mwaka mmoja uliopita. Tangu mwanzo mojawapo wa shinikizo kuu za waandamanaji ni kwamba nchi hiyo inahitaji katiba mpya ili kusuluhisha tatizo la ukosefu wa usawa katika jamii. Rais Piñera alisema kuwa katiba hiyo imewagawanya raia wa nchi hiyo na hivyo ipo haja ya kuifanyia marekebisho na kuanzisha mkondo mpya kwa nchi hiyo.

Raia wa Chile wapigia kura katiba ya iliyokuwa imepitishwa wakati wa enzi ya utawala wa kiimla

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *