Arteta awatuma Luiz na Ceballos nyumbani

Beki wa Arsenal David Luiz na kiungo Danni Ceballos walitenganishwa na wachezaji wenza na wakufunzi wa arsenal baada ya wachezaji hao kuzua rapasha katika kambi ya mazoezi ya arsenal.

 Taarifa ni kuwa Ceballos alimchezea kimabavu Luiz na kupelekea raia huyo wa Brazil kuupiga mpira kwa nguvu huku mpira huo ukimgonga pua Ceballos na kumwacha akivuja damu.

 Baada ya tukio hilo wachezaji hao walikuwa tayari kutupiana Makonde kabla ya kutenganishwa na kulazimishwa kuomba msamaha kwa lazima kabla ya kuamurishwa na mkufunzi Mikel Arteta kuondoka na kuelekea nyumbani.

 Aidha Ceballos kupitia ukurasa wake wa twitter amepinga kuwa tukio hilo lilitokea katika kambi ya mazoezi ya Arsenal.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *