Aliyemwacha mtoto katika afisi za TSC Wundanyi asakwa

Idara ya watoto mjini Wundanyi kaunti ya Taita Taveta kwa ushirikiano na washikadau mbalimbali eneo hilo wanaendeleza msako kumtafuta mama mmoja aliyemwacha mtoto mchanga nje ya afisi za tume ya kuajiri walimu Tsc eneo hilo.

Tukio hilo lililofanyika majira ya saa Mbili usiku,limewaacha wengi vinywa wazi hususan kina mama huku baadhi yao pamoja na mashirika mbalimbali ya kijamii yakiongozwa na sauti ya wanawake yakikashifu kitendo hicho.

Inakisiwa babake mtoto huyo mvulana,anayehudumiwa na madaktari katika hospitali ya kaunti ndogo ya Taita,huenda anafanya kazi katika afisi hizo alikowachwa.

Lidya Mwamberi ni Mwenyekiti wa Sauti Ya Wanawake mjini Wundanyi.

Hata hivyo amemshauri mama mhusika kujitokeza na kuwajibikia mwanawe mdogo wa masiku na kutafuta msaada mwafaka kwa mjibu wa sheria iwapo babake alikwepa kujukumika.

Haya yanajiri huku juhudi za kuwasaka wazazi wa malaika huyo asiye na hatia zikendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *