Aliyekua Kipa Wa Harambee Starlets Kuzikwa Oktoba 24

Aliyekuwa kipa wa Harambee Starlets Rosemary ‘Mara’ Kadondi atazikwa tarehe 24 mwezi huu nyumbani kwao Sori kaunti ya Homa Bay.

Taarifa hii imethibitishwa na naibu rais wa shirikisho la soka nchini FKF  Doris Petra Atieno.

Mara alifariki mwezi huu tarehe 4 kwenye hospitali ya St Francis ya mtaani Kasarani kaunti ya Nairobi alipokuwa akipokea matibabu baada ya kuugua kwa muda mfupi kabla ya  kifo chake alikuwa akihudumu kama meneja wa kutunza daluga za kuchezea kwenye kikosi hicho cha Harambee.

Nguli huyo amefariki akiwa na miaka 44 mnamo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *