Al Duhail wavunja Benki kwa Olunga

Al Duhail wavunja Benki kwa Olunga

Huenda ikawa mshambulizi wa harambee stars Micheal Olunga amejiunga na club ya Al Duhail Fc ya Qatar akitoka nchni Japan ndani ya club ya Kashiwa Reysol.

Kwa mujibu wa tarifaa iliochapishwa katika jarida la habari la Instagram la club ya Al Duhail ilionyesha picha ya mshambulizi huyo wa harambee stars akizinduliwa japo club hio bado haijachapisha taarifa kamili kuhusu uhamisho huo.

Tetesi nikuwa club ya Al Duhail alitoa shilling millioni 800 kupata sahihi ya Olunga kutoka Japan.

Olunga alitajwa kuwa mchezaji bora katika ligi ya Japan baada ya kufunga mabao 28 katika mechi  30 na kutajwa mchezaji bora katika J1 nchini Japan.

Mapema wiki Jana baada yatarifaa kutoka kuwa Olunga alikuwa nasakwa na club ya Al Duhail mshambulizi wa zamani wa Harambee stars Denis Oliech alimrai Olunga kujiunga na club ya Al Duhail na kutengeneza hela kwani kwa sasa umri wake umekwwnda sana na sio kijana mdogo tena.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *