Afariki Baada Ya Kulipukiwa Na Tairi

Mwanamume mwenye umri wa miaka 50 amefariki papo hapo baada ya tairi ya lori kulipuka eneo la  Diani kaunti ya Kwale.

Kulingana na ripoti ya polisi, marehemu David Mutua Kitheka alikuwa akiunganisha tairi hilo lilokuwa limejaa upepo  ambalo lililipuka ghafla, na kumuua papo hapo.

Polisi wamesema wahasiriwa wengine ambao bado hawajatambuliwa walifikishwa katika hospitali ya Kinondo wakiwa katika hali mbaya kufuatia kisa hicho.

Mwili wa marehemu umelazwa katika makafani ya hospitali ya  cha Kwale.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *