ADAK Yahamasisha Wanamichezo Kwale

Shirika la kupambana na utumizi wa dawa za kusisimua misuli nchini ADAK limeanzisha mchakato wakuwahamasisha wanamichezo nchini dhidi ya athari za utumizi wa dawa hizo.
Afisaa katika shirika hilo Martin Yauma aliyekuwa akizungumza na wanamichezo kaunti ya Kwale ameutaja utumizi wa dawa za kusimumua misuli kuwa haramu na ziko na athari nyingi za kiafya.
Yauma anasema kwamba wameeka mikakati yakuona kwamba utumizi wa dawa hizo humu nchini unakomeshwa akiutaja kuleta taswira mbaya kwa taifa licha kutambulika kispoti.
Ni kauli iliyoungwa mkono na Leyla Said refa wa ndondi nchini huku  akiitaka serikali ya kaunti ya  Kwale kukuza vipaji vya wanaspoti.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *