Yoshihide Suga Achaguliwa Kumrithi Shinzo Abe Japan

Chama tawala nchini Japan kimemchagua Yoshihide Suga kuwa kiongozi wake mpya kumrithi Shinzo Abe, kumaanisha kuna uwezekano mkubwa wa yeye kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo. Mwezi uliopita  Abe alitangaza kujiuzulu kwake kwa sababu za kiafya.  Suga, mwenye umri wa miaka 71, anahudumu kama mkuu wa mawaziri katika  serikali ya sasa na alitarajiwa na wengi kushinda kiti hicho. Anazingatiwa kuwa mwandani wa karibu wa Abe na kuna uwezekano kuwa ataendeleza sera za mtangulizi wake.  Suga ameshinda kura ya urais wa chama cha Liberal Democratic Party (LDP) kwa kupata kura 377 kati ya kura zote  534 kutoka kwa wabunge na wawakilishi wa kimaeneo. Kura nyingine itapigwa Jumatano bungeni ambapo kuna uwezekano kuwa Suga atachaguliwa waziri mkuu kutokana na wingi wa wanchama wa chama cha LDP bungeni. Suga atamalizia muda uliosalia wa hatamu ya sasa hadi uchaguzi utakapoandaliwa mwezi Septemba mwaka 2021.

Yoshihide Suga Aliyechaguliwa na Chama Tawala cha Japan Kuwa Kiongozi Wao Mpya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *