Watafiti wajitahidi kustawisha chanjo dhidi ya COVID-19

Watafiti wamepiga hatua muhimu katika kustawisha chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19, huku baadhi ya chanjo hizo zikiwa katika hatua za mwisho za majaribio yake, lakini chanjo kamili haitatolewa hadi mapema mwaka 2021.

Kulingana na mtaalamu mmoja wa shirika la Afya duniani (WHO). Mike Ryan, ambaye ni mkuu wa kitengo cha mipango cha dharura katika (WHO), anasema shirika hilo linajitahidi kuhakikisha kwamba dawa za chanjo zinagawanywa kwa usawa, lakini kwa wakati huu ni muhimu kuzuia maambikizi zaidi ya virusi vya ugonjwa wa COVID-19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *