wana Michezo kenya mashakani endapo mswada mpya utapita bunge

Uuzaji, umiliki au matumizi ya dawa za kusisimua misuli litakuwa kosa la uhalifu humu nchini.

Haya ni kulingana na mwenyekiti wa kamati ya michezo bungeni Peter Makau ambaye amesema kamti hio inapania kutunga sheria zitakazopitisha matumizi, uuzaji au umiliki wa dawa haramu michezoni kuwa kosa la jinai.

Mwezi July  waziri wa michezo Balozi Amina Mohammed alipendekeza  uuzaji, umiliki au matumizi ya dawa za kusisimua misuli kuwa kosa la uhalifu humu nchini.

 Hoja ilioungwa mkono na wengi wa washikadau wa michezo ikiwamo kamati ya michezo bungeni. Mbunge Peter Makau ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo amesema kuwa mswada huo utapitishwa bungeni

Iwapo mswada huo utapitishwa, Kenya itajiunga na mataifa mengine duniani ambayo yamepitisha sheria zinazofanya uuzaji, umiliki na matumizi ya dawa za kusisimua misuli kuwa kosa la uhalifu ikiwamo; Uchina, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Mexico na New Zealand miongoni mwa nyingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *