Wakulima Kifili walalamika kwa ukosefu wa wataalam wa kilimo mashinani

Wakulima kutoka kaunti ya kilifi wameendelea kulalamikia serikali ya kitaifa na ile ya kaunti hiyo kuingilia kati suala la ukosefu wa wataalam wa kilimo mashinani.

Mmoja wa wakulima hao kutoka eneo la shungwaya kaunti hiyo John Mutula amesema wanapitia changamoto nyingi za kilimo kwa sasa.

Hiyo ni kutokana na ukosefu wa maafisa wa kilimo kuzuru katika mashamba yao kuona kwamba wanawasaidia kutatua changamoto zinazowakumba ili kuboresha kilimo chao.

Wakati uo huo amesema maafisa hao wa kilimo huonekana pekee wakati wa mikutano ya wakulima hali inayowalazimu kutumia ujuzi wao pekee katika kujisaidia katika ukulima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *