Wakali wa mashambulizi na Ulizi wakutana

Mechi kati ya manchester city na Real Madrid usiku wa leo itavikutanisha vilabu viwili vinavyo jivunia safu kali ya mashambulizi na safu kali ya mabeki.

Musimu huu Manchester city ndio club iliofunga mabao mengi wakiwa wamefunga jumla ya mabao 146 ambapo inashiria kuwa Kevin De Bruyne Rahim Sterling, Sergio Kun Aguero, Gabriel Jesus ndio wachezaji wabunifu zaidi barani ulaya.

 Nao real Madrid ni wapili katika ya vilabu vilivyofungwa mabao macheche barani ulaya wakiwa wamefungwa mabao 41.

 Mabeki Sergio Ramos, Rapheal Varane, Dani Carvajal,Eder Militao na Marcelo musimu huu wamekuwa mabaki imara real amepiga mechi 19 musimu huu bila ya kufungwa nao.

Leo Usiku Ugani Etihad nchni Ugereza Vilabu hivyo vitakuwa vinawania kupata nafasi ya kufuzu robo fainal ya dimba la klabu bora bara ulaya.

 Mkondo wa kwanza ugani Santiago Barnabeu Machester city alipata ushindi wa 2-1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *