Wakaazi wa petangua wataka naibu chifu kuhamishwa kwa madai ya kudona vifaranga

Wakazi wa kata ndogo ya Petangua eneo la Ganze kaunti ya Kilifi wanaitaka serikali kumuondoa mamlakani naibu chifu wa eneo hilo kwa madai ya kuwa na maadili potofu.

Wakiongozwa na Karani Charo Kavula wakazi hao wanadai kuwa afisa huyo tawala amekuwa akishiriki ngono na watato wa shule pamoja na mabibi za watu.

Kulingana na mwenyekiti wa shirika la sauti ya wanawake eneo hilo Judith Uchi visa vya viongozi wa utawala kuwabaka Watoto sasa vimekithiri eneo hilo.

Uchi ametoa wito kwa serikali na mashirika ya kutetea haki za wanawake na Watoto kuingilia kati ili kuhakikisha washukiwa wa visa hivyo wanachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa upande wake naibu chifu huyo Gilbert Kiti amekanusha madai hayo na kusema kuwa hatua hiyo imesababishwa na mzozo wa shamba unaoendelea baina ya koo mbili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *