Wahudumu wa Afya wa Milki Za Kiarabu Kupata Chanjo

Muungano wa milki za kiarabu umetoa idhini ya dharura ya utumiaji chanjo ya virusi vya corona kwa wahudumu wa afya .  Awamu ya tatu ya majaribio ya chanjo hiyo iliyotengenezwa na China ilianza kutekelezwa nchini humo mwezi Julai na bado haijakamilika.    Halmashauri ya kitaifa ya kushughulikia masuala ya dharura na majanga katika muungano wa UAE, ilisema kupitia mtandao wa Twitter kwamba chanjo hiyo itapatikana kwa watu hao ambao wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa virusi hivyo. Halmashauri hiyo ilisema chanjo hiyo haijakuwa na madhara yoyote baada ya kufanyiwa majaribio kwa watu elfu-31 waliojitolea. Takriban chanjo 140 ziko katika hatua za mwanzo za utengenezaji kote duniani, na kadhaa zinafanyiwa majaribio kwa watu.  Zingine chache zimefikia awamu muhimu au ziko katika awamu ya tatu ya majaribio na hakuna zozote ambazo kufikia sasa zimethibitishwa kuwa salama kabisa kwa matumizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *