Wafanyikazi wa kaunti kuenda Likizo ya Lazima kote nchini

Mwenyekiti wa baraza la magavana nchini Wycliffy Oparanya amewaagiza magavana wote kote nchini kuwapatia wafanyikazi wao likizo ya lazima ya wiki mbili kuanzia hapo kesho tarehe 17 mwezi septemba.

Oparanya amesema hospitali hazitafungwa japo amewaagiza magavana kuwaeleza wauguzi kutowapokea wagonjwa wapya kuanzia kesho.

Mwenyekiti huyo amesema mvutano unaoshuhudiwa katika bunge la seneti umechangia ukosekanaji wa fedha katika serikali za kaunti na kukwamisha miradi mingi ya maendeleo.

Kwa upande wake waziri wa fedha na hazina ya kitaifa Ukur Yattani amesema sheria imemfunga kiasia cha kuwa hana uwezo wa kutoa fedha zozote kwa kaunti kabla ya bunge la seneti kukubaliana njia mwafaka itakayotumiwa kugawanya fedha hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *