Wabunge wapwani watakiwa kukomesha malumbano nje ya bunge.

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharrif Nassir amewataka wabunge wenza kutolumbana kwa sababu zisizokuwa na msingi,kuhusiana na miradi katika ukanda huu wa pwani baada ya shutuma kutoka kwa baadhi ya wabunge wa pwani.

Kauli hii inajiri baada ya baadhi ya viongozi hasa wabunge kupiga kelele nje ya bunge,kwa masuala ambayo amedai laity yangeshughulikiwa ndani ya bunge yangepata suluhu.

 Aliyasema hayo baada ya kuanzisha mradi wa mafunzo kwa vijana kujikimu na mbinu za biashara kupitia hazina ya CDF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *