Ugavi wa mapato kwa serikali za kaunti wazidi kuligawanya bunge la seneti.

Bunge la  Senate bado limegawanyika kuhusu mfumo bora wa kugawa mapato kwa kaunti 47 kabla ya kikao cha leo .

Bunge la  Senate bado limegawanyika kuhusu mfumo bora wa kugawa mapato kwa kaunti 47 kabla ya kikao cha leo .

Bunge hilo linatarajiwa kujadiliana na kupiga kura kuhusiana na ripoti ya kamati yake maalum kama ilivyofanyiwa marekebisho huku kukiwa na mipango ya kuwasilisha azimio la kutaka mabunge mawili kurekebisha sheria ya mapato ili kuruhusu kaunti kupata asilimia hamsini ya mgao wa kila mwaka iwapo bunge la  Senate litakosa kutatua swala hilo.

Juhudi za kuafikia makubalino kuhusu mfumo wa kugawa mapato ziliambulia patupu baada ya spika wa bunge la Senate  Kenneth Lusaka kukataa kuandaa mkutano wa  kamukunji kujadili swala hilo.

Kwa mujibu wa baadhi ya maseneta, mfumo wa tume ya ugavi wa mapato nchini ulikuwa wa kisiasa.

Wajumbe hao wameshindwa mara tisa kupitisha mfumo huo ambao ungebaini namna kaunti zingegawana shilingi bilioni 316.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *