Ufujaji Wa Pesa Watajwa Kukwamisha Ujenzi Wa Chuo Cha Utalii Kilifi

Baadhi ya wanasiasa kaunti ya Kilifi wanadai kuwa zaidi ya shilingi bilioni 2.8 zilifujwa katika mradi wa ujenzi wa chuo cha utalii cha Ronald Ngala eneo la Vipingo kaunti hio baada ya kukwama.
Mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya amedai kuwa pesa hizo zimekuwa zikilipwa wadau mbali mbali wanaohusika na ujenzi huo kwa manufaa binafsi ya watu wachache.
Baya amesema chuo hicho kilitarajiwa kukamilika tangu mwaka wa 2017 lakini idara husika haijatekeleza majukumu yake ipaswavyo.
Hata hivyo mbunge huyo ameahidi kusimama kidete katika kuhakikisha mradi huo unakamilika ili wananchi waweze kufaidika.
Amesema kucheleweshwa kwa mradi huo kumechangia pakubwa katika kudorora kwa sekta ya utalii nchini kutokana na uhaba wa wafanyikazi waliohitimu katika Nyanja hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *