Ubovu wa barabara waathiri huduma shimbahills.

Wakaazi wa Barcelona katika kijiji cha Mwaweche huko Msambweni kaunti ya Kwale wamelalamikia miundo msingi duni ambayo imeathiri pakubwa shughuli za usafiri katika eneo hilo.

Wakiongozwa na Philomena Mutiso, wakaazi hao wameitaka serikali kuikarabati barabara ya Shimba hills na ile ya Magaoni ambayo wanasema kuwa haipitiki wakati wa msimu wa mvua.

Vile vile, wamebainisha kwamba daraja la miembeni linalounganisha eneo hilo na Shimba hills liko katika hatari ya kuporomoka kwa kuwa hali yake ni mbaya.

Kutokana na hali hiyo, sasa wakaazi hao wanataambika kupata huduma za matibabu kutokana na umbali wa kituo cha afya cha Mwapala.

Hali hiyo imeathiri pia elimu ya watoto wao waliokuwa wakilazimika kutembea mwendo mrefu wa kilomita mbili wakienda shuleni katika eneo la Kubo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *