Taita Taveta: SUPKEM yawashauri wakenya kufuta maagizo ya Covid-19

Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Nchini SUPKEM Kaunti ya Taita Taveta Mohammed Washalla amewashauri wakenya kuzingatia sheria zilizowekwa katika maeneo ya ibada ili kukabili ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona.

Washalla ameipongeza serikali kwa kuruhusu kufunguliwa kwa maeneo ya ibada baada ya kufungwa kwa zaidi ya miezi mitatu.

Kiongozi huyo vile vile amewashauri waumini kuzingatia sheria iliyowekwa kwa wanaofaa kuhudhuria nyumba za ibada.

Hata hivyo ameelezea changamoto wanazokumbana nazo viongozi wa makanisa na misikiti iliyo na idadi kubwa ya waumini.

Kadhalika ameitaka serikali kutathmini upya sheria hizo na kulegeza baadhi ya sheria ili kuruhusu wakenya wengi kuhudhuria ibada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *