Taita Taveta: Baba ambaka mwanawe

Mwanamume mmoja kutoka kijiji cha Mwambalo Kata ya Mghange eneo bunge la Wundanyi kaunti ya Taita Taveta anazuiliwa na polisi katika kituo cha polisi cha maghange kwa madai ya kumbaka Mwanawe.

Mwanamume huyo kwa jina Mark Mlango Mghalu wa umri wa miaka 40 anadaiwa kumbaka msichana wake wa umri wa miaka 5 nyumbani kwake usiku wa kuamkia Jana.

Kulingana na baadhi ya majirani ambao hawakutaka majina yao yatajwe wanasema mshukiwa aliingia nyumbani kwake usiku na kumfurusha mkeo nje na kufunga Mlango kabla ya kuanza kumtendea mwanawe uovu huo.

Mtoto huyo sasa anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Wesu alikokimbizwa baada ya tukio hilo huku mshukiwa akitazamiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote ili kujibu mashtaka yanayomkabili.

Haya yanajiri huku maafisa wa utawala katika eneo hilo wakiendelea na mikakati mbalimbali za kukabiliana na ongezeko la visa vya dhuluma za kijinsia sawa na mimba za mapema kwa wasichana hususan majira haya ya chamko la ugonjwa wa corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *