Sudan yagundua kaburi la halaiki la tangu mwaka 1990

Serikali ya Sudan imegundua kaburi la halaiki la tangu mwaka 1990.

Mwanasheria Mkuu alisema kuwa kaburi hilo la halaiki lilikuwa na mabaki ya miili ya maafisa 28 wa kijeshi wanaoaminika kuhusika kwenye jaribio la kupindua serikali ya aliyekuwa Rais Omar al-Bashir.

Serikali ya Bashir ilitibua jaribio la jeshi la kupindua serikali mwaka 1990 huku ripoti nyingi zikisema kuwa maafisa waliohusika waliuawa.

Kwa sasa anakabiliwa na mashtaka kuhusiana na mapinduzi ya serikali yaliyotekelezwa na jeshi yaliyomweka mamlakani mwaka 1989.

Iwapo atapatikana na hatia rais huyo wa zamani aliyetawala Sudan kwa miaka 30 huenda akahukumiwa kifo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *