Serikali Yahimizwa Kuwanunulia Sodo Wasichana Washule

Wazazi kutoka  eneo la Malanga kaunti ya Kilifi wameitaka serikali ya kitaifa na ile ya kaunti kuanzisha utoaji sodo kwa wasichana.

Sidi Charo, ambaye ni mmoja wa wazazi hao amedokeza kuwa  huenda idadi kubwa ya wasichana wakakosa kurudi shule kufuatia wengi kutungwa mimba.

Kwa upande wao wasichana hao wamesema wakati mwingi hulazimika  kutumia kila mbinu ikiwemo kushiriki mapenzi ili waweze kupata sodo, hii ni baada ya mpango wa utoaji sodo shuleni kusimama baada ya shule kufungwa kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Wazazi na wsichana hao sasa wameipa changamoto Serikali kuendelea na mpango huo wa utoaji sodo licha ya shule kufungwa, wakitaka mpango huo kufanikishwa kupitia machifu na wazee wa vijiji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *