Serikali Ya Kaunti Ya Kwale Yahimizwa Kukamilisha Ujenzi Wa Barabara

Wakaazi wa   eneo la Kona ya Musa  eneo la  Ukunda  kaunti  ya Kwale  wanaitaka serikali ya kaunti  hiyo kuharakisha  kukamilisha   ujenzi wa  barabara  ya  Babla Mvindeni kwa kile wanachodai kuwa imetatiza pakubwa shughuli za usafiri katika eneo  hilo.

Wakiongozwa na Maina Peter katika kikao na wanahabari amesema kuwa kuwekwa kwa matuta hayo katika barabara hiyo bila  kujengwa imewatatiza pakubwa kiusafiri.

Sasa wenyeji wanaitaka serikali ya kaunti hiyo kuharakisha haraka upesi kukamilisha ujenzi ili shughuli za kawaida ziweze kurejea.

Tetesi za wakaazi hao zinajiri wakati mwanakandarasi anasemakana kuweka matuta ya mawe na  mchanga  katika barabara hiyo kwa zaidi ya wiki tatu sasa bila kuikarabati barabara hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *