Serikali Sambamba ya Mashariki ya Libya Kujiuzulu

Serikali sambamba ya mashariki ya Libya imewasilisha barua ya kujiuzulu kufuatia maandamano  ya kulalamikia kudorora kwa hali za maisha na ufisadi. Kwenye maandamano ya hivi punde ,waandamanaji jijini  Benghazi waliteketeza makao makuu ya kamanda wa kijeshi, Khalifa Haftar. Waandamanaji hao pia walipigana kwenye ngome yake ya Al-Maj kwa mara ya kwanza. Msemaji wa jenerali huyo ameelezea  kwamba utawala umeunga mkono maandamano ya amani japo hautaruhusu wanamgambo wa kigaidi Pamoja na wale wa kiislamu kuingilia kati. Kufikia sasa,mandamano dhidi ya hali hizo nchini humo yameshamiri katika jiji kuu Tripoli ambako ni makao makuu ya serikali inayotambuliwa na umoja wa kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *