Ramadhan Kajembe amempoteza mke wake wa kwanza Aziza

Aliyekua mbunge wa Changamwe na waziri msaidizi Ramadhan Kajembe amepata pigo lengine hii ni baada ya mke wake wa kwanza Aziza Kajembe kuaga dunia mapema leo katika hospitali ya Pandya hapa mjini.


Kifo cha mke wake wa pili kinajiri miezi michache tu baada ya mbunge huyo wa zamani kumpoteza mkewe wa pili kwa jina Zaharia Kajembe mnamo mwezi Machi mwaka huu.


Mama Zaharia alikua mama mkwe wa mbunge wa Jomvu Badi Twalib.


Ikumbukwe pia mnamo mwaka 2017 mheshimiwa Kajembe aliweza kumpoteza mtoto wake wa kwanza Seif Kajembe.


Hapa Pwani Fm twasema makiwa kwa familia ndugu na marafiki wa Ramadhan Kajembe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *