Oguna amethibitisha kuwa na virusi vya Korona

Msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna amethibitisha kuwa na virusi vya Korona. Kupitia ukurasa wake wa twitter, Oguna amesema alirejea jijini Nairobi hivi majuzi baada ya kwenda kazi nje ya jiji na akahisi dalili chache zilizofanana na za virusi vya corona kabla ya kupimwa na kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo.

Oguna alisema anapokea matibabu katika hospitali ambapo amejitenga. Amethibitisha kwamba familia yake ipo salama na kwamba harakati za kuwatafuta watu aliotangamana nao zinaendelea.

Amerai wakenya kutembelea vituo vya afya iwapo watajihisi vibaya badala ya kusubiri kwa muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *