NHIF kutoa huduma kwa wagonjwa wa Covid-19 katika hospitali za serikali

Hazina ya kitaifa ya matibabu imesema kwamba itatoa huduma za kimatibabu kwa wagonjwa walioambukizwa ugonjwa wa Korona katika hospitali za serikali.

Kwenye taarifa, mkurugenzi mkuu wa hazina hiyo, Peter Kamunyo amesema hatua hiyo itahakikisha wale walioambukizwa ugonjwa huo wananufaika.

Hospitali zitakazotoa huduma hiyo ni pamoja na Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta, Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kenyatta pamoja na Hospitali ya Mbagathi.

Hospitali zingine ni zile zilizopendekezwa na wizara ya afya. Watoaji wa bima ya afya wamekua wakiwarejesha nyumbani wagonjwa licha ya kuwa wana maelfu ya pesa kwenye bima kutokana na kwamba walioambukizwa ugonjwa wa Covid-19 wanafaa kujilipia gharama ya matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *