Mwanasayansi wa Kichina atorokea ubalozi mdogo ulioko San Francisco

Mwanasayansi mmoja wa China anayeshukiwa nchini Marekani kupata visa kwa njia ya udanganyifu na kuficha uhusiano wake na jeshi ametorokea Ubalozi mdogo wa China ulioko San Francisco.

Waendesha mashtaka wanadai kwamba kesi hiyo ni sehemu ya mpango wa serikali ya China wa kutuma wanasayansi wa kijeshi kuendesha shughuli za ujasusi nchini Marekani.

Hapo jana, serikali ya Trump iliamurisha kufungwa kwa ubalozi mdogo wa China mjini Houston, ikisema unashiriki katika wizi wa haki miliki.

Msemaji wa Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya China, Wang Wenbin, ameshtumu serikali ya Marekani kwa kutumia visingizio kupunguza na kuhangaisha wasomi raia wa China nchini humo.

Alisema kuwa China sharti ichukue hatua zinazofaa na kulinda haki zake. Kufuatia mzozo kuhusu kufungua kwa ubalozi huo mdogo, Rais Donald Trump alitisha kufunga balozi zaidi ndogo za China.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *