Messi amezidi Ronaldo dollar millioni 9

Nahodha wa Barcelona lionel Messi amempiku Cristiano Ronaldo na kuwa mchezaji wa soka anayepokea mshahara mkubwa kote duniani kwa kipindi cha  muda wa mwaka mmoja kulingana na jarida la forbes.

Messi alipokea dolla millioni 126 kwa kipindi cha muda wa miezi 12 iliopita huku Ronaldo akipokea dolla million 117.

 Mashabiki wa wawili hao wamekuwa na uhsama mkubwa na kuwalinganisha ndani na nje ya uwanja.

Mkataba wa Messi ugani camp Noue unapa dolla millioni 80 kwa mwaka huku akiwa na udhamini na makapuni kama vile AdidasGatoradeHuaweiMastercardPepsi

Messi pia anamiliki duka la mavazi mjini Barcelona na ni kati ya maduka tajika barani ulaya.

Kwa upande wake Critiano  Ronaldo anamkatapa wad olla millioni 34 na Juventus na amesaini mkataba wa maisha na kampuni ya nike ambao wanamlipa dolla millioni 19 kila mwaka hadi atakapo fikisha umri wa miaka 73.

Ronaldo pia anamiliki hoteli za kifahari linalojulikana kama CR7 hotels na pia anamiliki kampuni ya kuuza chupi, na udhamini wa makapuni mengine mengi.

Hii hapa orodha ya wachezaji waliopokea fedha nyingi chini ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Forbes’ top 10 highest-paid footballers:

1. Lionel Messi – $126m (£98m) 
2. Cristiano Ronaldo – $117m (£91m)
3. Neymar – $96m (£74.7m)
4. Kylian Mbappe – $42m (£32.6m)
5. Mohamed Salah – $37m (£28.8m)
6. Paul Pogba – $34m (£26.5m)
7. Antoine Griezmann – $33m (£25.7m)
8. Gareth Bale – $29m (£22.6m)
9. Robert Lewandowski – $28m (£21.8m)
10. David De Gea – $27m (£21m)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *