Matiang’i anasema mfumo wa dijitalii ndio njia mwafaka ya kushughulikia changamoto za usalama

Waziri wa Usalama wa Taifa, Dr. Fred Matiang’i anasema mfumo wa dijitalii ndio njia mwafaka ya kushughulikia changamoto za usalama zinazokumba taifa hili.

Akiongea leo alasiri wakati wa kuzindua kitabu cha kidijitalii cha kunakili matukio yanayoripotiwa katika vituo vya polisi al maarufu OB, Matiang’i alipongeza matumizi ya mfumo wa kidijitalii katika idara ya polisi akisema huduma nyingi za serikali sasa zinatolewa kupitia majukwaa ya kidijitalii jinsi alivyoahidi rais Uhuru Kenyatta kwenye ahadi zake za kampeni ya uchaguzi.

Alimwagiza Inspekta Jenerali wa Polisi, Hilary Mutyambai kuhakikisha maafisa wa polisi wanapata mafunzo kuhusu mfumo huo mpya katika muda wa miei 18 ijayo.

Alisema hatua hiyo itahakikisha ukusanyaji bora wa takwimu ambazo zinaweza kupatikana haraka katika maandalizi ya mikakati ya kushughulikia haraka visa vya uhalifu.

Alisema swala la faili kutoweka ambalo huathiri utoaji huduma kwa umma halitakuwepo tena.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *