Mashirika Mbalimbali yashirikiana kuzima Moto kwenye mbunga ya Tsavo Magharibi

Shirika la huduma kwa wanyama pori nchini (KWS) linashirikiana na vikosi vya ulinzi wa Kenya (KDF), shirika la huduma za vijana kwa taifa (NYS), shirika la huduma za misitu nchini (KFS), utawala wa kaunti ya Taita Taveta, washirika wa maswala ya uhifadhi na pia jamii katika juhudi za kuuzima moto wa hivi punde kwenye mbuga ya kitaifa ya Tsavo Magharibi.

Makundi ya ardhini na pia angani yamepelekwa kukabiliana na moto huo ambao ulianza katika eneo la Sheikdam jumamosi alasiri huku ikishukiwa kwamba ulianzishwa makusudi na wateketezaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *