Mashindano ya tenisi ya Madrid Open yamefutiliwa mbali

Mashindano ya tenisi ya Madrid Open yamefutiliwa mbali kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona katika eneo hilo.

Mashindano hayo ambayo awali yalikuwa yamepangwa kuandaliwa mwezi Mei yangeandaliwa baina ya tarehe 12 na 20 mwezi ujao katika uwanja wa Magica.

Baada ya kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Uhispania, serikali ya jijini Madrid imependekeza mashindano hayo ya tenisi ya Madrid Open kufutiliwa mbali.

Kulingana na takwimu zilizotolewa kumekuwa na visa 1500 vya maambukizi ya virusi vya Corona kila siku nchini humo katika kipindi cha juma lililopita na kwa jumla Uhispania imerekodi vifo elfu-28 vilivyotokana na ugonjwa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *