Maseneta watishia kuwaadhibu magavana watakaofunga kaunti

Wenyekiti wenza wa kamati ya seneti iliyobuniwa kutatua mzozo kuhusu mfumo mpya wa ugavi wa mapato Moses Wetang’ula na Johnson Sakaja wamehakikishia serikali za kaunti kwamba mzozo huo wa kifedha utatatuliwa.

Kamati hiyo ya wanachama 12 itakutana leo asubuhi kutafuta suluhu baada ya rais Uhuru Kenyatta kuahidi shilingi bilioni 50 zaidi kwa serikali za kaunti katika mwaka ujao wa matumizi ya fedha za umma.

Maseneta hao wawili walitoa hakikisho hilo huku wenzao wakimkashifu mwenyekiti wa baraza la magavana Wycliffe Oparanya,hasa kwa taarifa yake kwa serikali za kaunti kufunga taasisi zao za afya pamoja na ile taarifa ya awali ambapo alitishia kuitisha kuvunjiliwa mbali kwa bunge la seneti endapo litashindwa kuafikiana kuhusu mfumo bora wa ugavi wa mapato.

Maseneta hao walitishia kumuadhibu gavana yoyote atakayetekeleza agizo hilo la Oparanya.

Wakihoji jinsi serikali za kaunti hutumia fedha zinazokusanya,maseneta hao walimlaumu waziri wa fedha Ukur Yattani kwa uhaba huo wa kifedha katika kaunti.

Walisema waziri huyo ameshindwa kutekeleza ushauri wa mahakama mwaka jana ulioruhusu serikali za kaunti kupata nusu ya mgao wao wa kifedha. iqua”,”serif”;mso-bidi-font-family:Tahoma; color:black;background:white’> Covid-19 liliathiri ukusanyaji wa mapato kwenye kaunti hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *