Masauti aatarajiwa kuangusha balaa zito

Msanii Masauti mkali wa ‘kiboko’,’ipepete’ aatarajiwa kuangusha balaa zito hii baada ya hivi juzi katika mahojiano na mtangazaji tajika humu nchini Gates mgenge kupitia ‘Gates live online show’ ambapo Masauti alidokeza kua kwenye Ep yake (001EP) apania kufanya nyimbo na msanii wa kike mkubwa tuu sana Tanasha Donna ambae tayari washaonekana kwenye lokesheni kadhaaa mjini mombasa.Video inayohusisha mtayarishaji ‘Hanscana’toka nchini Tanzania,ambapo pia kwenye utayarishaji wa audio hio Kwa jina ‘liar’yaani ‘Muongo’ amehusika Shirko toka pande za Mombasa ndani ya studio za ‘Shirko Media’.Kwa upande wa Tanasha Donna ambaye wengi twamfahamu kama aliyekua mpenzi wa msanii tajika Duniani apa namuongelea ‘Diamond Platnumz’ yaani baby mama wake wa zamani azidi kuonyesha uwezo wake kupitia kipaji chake,kwa sasa atamba na nyimbo yake’SAWA.’ Tanasha alizungumzia nyimbo hio kua aliitoa kuonyesha upendo,amani na pia umoja kwake na hata kwa watu baki pia,ngoma hio(Sawa) ambayo pia ipo kwenye Ep yake(Donna Tella EP) ilionekana kumpa moyo Tanasha baada ya kufikisha watazamaji millioni moja na nusu(1.5)kwenye mtandao wa YouTube katika kipindi cha mwezi mmoja. Nukuu…`kufikisha watazamaji millioni moja unusu ndani ya mwezi mmoja kwangu ni mafankio makumbwa sana izigatiwe kua sio rahisi kwa mwanamke kwenye hii tasnia ya mziki’japo nukuu ilikua refu ila hayo ni baadhi ya maneno ya Tanasha,pia aliongeza kua japo wimbo huo wa ‘Sawa’ haukua kwa mazingira yake alibidi autoe ili kuhamasisha ama kutia moyo watu wengine wanaopitia hali ngumu za kimaisha.Asanteni Afrika mashariki kwa kuwezesha na kupokea wimbo huu(Sawa) vizuri na hata nje ya Afrika pia japo kuna wengine walidhani sitaweza peke yangu~Tanasha alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *